Kenya yatamba katika mita 3,000 kuruka viunzi - IAAF

Athletics - World Athletics Championships - Doha 2019 - Women's 3000 Steeplechase Final - Khalifa International Stadium, Doha, Qatar - September 30, 2019. Kenya's Beatrice Chepkoech celebrates winning the race. REUTERS/Ahmed Jadallah
Athletics - World Athletics Championships - Doha 2019 - Women's 3000 Steeplechase Final - Khalifa International Stadium, Doha, Qatar - September 30, 2019. Kenya's Beatrice Chepkoech celebrates winning the race. REUTERS/Ahmed Jadallah
NA NAOM MAINYE

Beatrice Chepkoech aliishindia Kenya medali ya dhahabu ya pili Jumatatu usiku kwa kuibuka mshindi katika finali ya mita 3000 kuruka viunzi na maji katika mashindano ya riadha ya ubingwa wa dunia yanayoendelea mjini Doha- Qatar.

Mkenya mwingine Hyvin Kiyeng Jepkemoi alimaliza katika nafasi ya nane katika mita 3000. Eunice Sum alishindwa kutamba na kumaliza wa tano kwenye finali ya mbio za mita 800 huku Jacob Kiprop na Nicholas Kimeli wakimaliza katika nafasi ya sita na nane mtawalia kwenye finali ya mita 5000.

Kufuatia matokeo haya Kenya inashikilia nafasi ya nne katika jedwali la mashindano ya ubingwa wa dunia IAAF yatakayokamilika tarehe 6/10/2019 mjini Doha-Qatar. Kenya ina jumla ya medali tatu kufikia sasa, mbili za dhahabu na moja ya shaba. Marekani wanaongoza jedwali kwa jumla ya medali 13, nne za dhahabu, saba za fedha na mbili za shaba.

Uchina ni wa pili wakiwa na jumla ya medali sita, mbili za dhahabu, mbili za fedha na mbili za shaba huku Jamaica wakiwa katika nafasi ya tatu kwa jumla ya medali nne, mbili za dhahabu, mbili za fedha.