Kenya yawaruhusu raia wa Tanzania kuingia nchini bila kuhitajika kwenda karantini (Orodha)

Kenya siku ya jumanne imetoa orodha ya mataifa ambayo raia wake wanaruhiusiwa kuingiaa nchini bila kuhitajika kwenda karantini kwa siku 14 . Hatua ya hapo awali ya Kenya kuwahitaji watanzania kwenda karantini wanapowasili kenya iliifanya Tanzania kulipiga marufuku shirika la  safari za ndege nchini KQ dhidi ya kufanya safari zake hadi katika taifa hilo Jirani .

Kulegezwa kwa masharti hayo kuhusu karantini kunaashiria kwamba kenya ina matumaini kwamba visa vya ugonjwa wa corona katika nchi hizo vimethibitiwa . Tanzania haijakuwa ikitoa iaddi ya wagonjwa wa corona tangu mwezi Aprili na kuzua hofu miongoni mwa mataifa  mengine ya afrika mashariki kwamba utawala wa Rais Magufuli haujachukua hatua zifaazo kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo .

Siku ya jumapili rais Uganda Yoweri Museveni na msafara wake walilazimika kuvlia barakoa na kutilia mkazo kanuni zote za kukabiliana na ugonjwa huo walipozuru Tanzania kwa hafla ya kusainiwa kwa  makubaliano ya kujenga bomba la usafirishaji wa mafuta  kutoka Uganda hadi katika bandari ya Tanga ,nchini Tanzania .