Kesi ya NYS imehamishwa katika mahakama mpya ya ufisadi

Picha: Maktaba

Kesi ya wizi wa shilingi milioni 791 za shirika la NYS imehamishwa hadi katika mahakama mpya ya kupambana na ufisadi. Kesi hiyo iliyowasilishwa na shirika la kurejesha mali Iliyoibwa dhidi ya Ben Gethi na washukiwa wengine ilifaa kusikizwa ili uamuzi utolewe iwapo Josephine Kabura alifaa kujumuishwa.

Hayo yakiarifiwa, mtaalam wa masuala ya kisiasa Mutahi Ngunyi amekanusha kuwahi kukutana na mshukiwa wa sakata ya NYS Josephine Kabura. Ngunyi hata hivyo amesema aliwahi kumwonya aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru kwamba bidhaa zilizonunuliwa kwa mradi wa usafishaji wa mtaa wa kibera zilikuwa zimeongezwa bei kupindukia.