Kesi ya uchochezi dhidi ya Kiunjuri yatupiliwa mbali

Picha: Twitter;

Kesi ya uchochezi dhidi ya Mwangi Kiunjuri, aliyeteuliwa kuwa waziri wa ugatuzi imetupiliwa mbali.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko amemwandikia barua mkuu wa CID Ndegwa Muhoro akitaka faili za kesi ya Kiunjuri lakini Muhoro akamjibu kwamba faili hizo hazipo na kesi dhidi ya Kiunjuri haiwezi kuendelea.

Kiunjuri hata hivyo anaweza kukamatwa na kushtakiwa upya endapo ushahidi zaidi utapatikana.