Khalwale awalaumu Wetangula na Mudavadi kwa Mariga kufeli Kibra

Seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale amewalaumu kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi na Seneta Moses Wetangula kwa kile anasema ni 'kumharibia kura Mariga' katika uchaguzi mdogo wa Kibra uliofanywa Alhamisi.

Khalwale ambaye alikuwa na wakati mgumu katika uwanja wa DC Kibra baada ya kufurushwa na wakaazi ameelekeza masaibu yake kwa viongozi hao.

Aidha alilalamikia fujo zilizoshuhudiwa katika eneo hilo kuwa chanzo cha wanawake kuogopa kujitokeza katika vituo vya kupigia kura.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Khalwale anasema kwamba hakukuwa na umuhimu wagombea wa Ford Kenya Khamisi Butichi na mwenzake wa ANC Eliud Owalo kushirki katika kinyang'anyiro hicho licha ya kwamba tayari Mariga alikuwa debeni.

https://twitter.com/KBonimtetezi/status/1192688191192682497?s=20

Alisema kwamba kura 5,275 alizopata Eliud Owalo na kura 260 za Khamisi Butichi zingemfaidi Mariga.

Matokea rasmi ya uchaguzi huo uliorodhesha Okoth Imran wa ODM kwa kura 24,636 huku Mariga akiwa wa pili kwa kura 11,230.

Jumla ya kura 41,984 zilipigwa katika vituo vyote vya Kibra huku idadi rasmi  ya wapiga kura ni 11,658.