Kibaki alinitajirisha nikiwa na miaka 16. Mwanamziki Single L afunguka

Mwanamziki wa kaunti ya Meru, Bi Single L asema kuwa, aliyekuwa rais wa kenya, Mwai kibaki alimtajirisha na kumfanya milionea akiwa na miaka 16.

Lynn Kendi ambaye jina lake la usanii ni Single L, alifunguka na kusema kuwa, anamheshimu na anajivunia aliyekuwa Rais, Bwana Mwai Kibaki kwani serikali yake ilitukuza na kusaidia wanarika kukuza talanta yao.

Zaidi ya hayo, Single L alisema kuwa, wakati huo alipotoa wimbo wake  wa kwanza, alilipwa pesa nyingi sana mpaka ikafika wakati alikuwa anashangaa atazifanyia pesa zile kazi gani.

''Nililipwa hadi nikashangaa nitapeleka wapi hela hizo," Alisema.

Vilevile, Single L alisema kuwa, alitumia pesa hizo kujilipia karo kwani hakuna mtu yeyote aliyekuwa anasimamia masomo yake, iwe jamii na ata wazazi wake.

Binti huyu alijieleza na kusema kuwa, mama yake wa kambo alikuwa amemkana na baba yake mzazi akakataaa kugharamia masomo yake, kitu ambacho kilimfanya abadilishe shule mara kwa mara alipokuwa kwenye shule ya upili.

Vilevile, alifunguka na kusema kuwa, kuna wakati mmoja mwalimu mkuu wa shule aliyokuwa, alitokwa na machozi baada ya kumpigia baba yake simu na kumwambia kuwa, anafaaa kumlipia karo mtoto wake na bwana huyu akajibu na kusema kuwa, hana mtoto kama huyo.

Hata hivyo, binti huyu alisema kuwa, alimsamehea baba yake na sasa wako sawa.

Vilevile, Single L alishinda tuzo la Mwafaka Award mwaka wa 2016 na akasema kuwa, tuzo hili lilimpa moyo sana wa kumfanya aweze kujiaminia sana.

Licha ya hayo, Single L alisema kuwa, tuzo hili lilimfanya aamini kuwa, kila kitu kinawezekana  kama mtu anataka afaulu. Aisee! penye nia, pana njia.

Binti huyu ni bibi ya mwanaume mmoja, bwana Keith Mureithi  na pamoja wambarikiwa na watoto wawili.

Single L alimaliza na kusema kuwa, amejijenga mwenyewe na hana mwanamziki yeyote anayemtazamia lakini anapenda mziki mzuri.