Rais mstaafu Mwai Kibaki hayupo hospitalini .katibu wake wa kibinafsi Ngari Gituku amesema ingawaje ni kweli kwamba kibaki alikuwa hospitali maajuzi ,ilikuwa ni uangalizi wa kawaida na hajalazwa .
Gituku ametaja kama ‘kuongezwa chumvi’ kwa ripoti katika vyombo vya habari kwamba Kibaki amekuwa hospitalini kwa siku kumi . Amesema Kibaki alitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani .
Msaidizi huyo wa Kibaki amesema hapafai kuwa na hofu wakatu mtu mashuhuri anapopelekwa hospitalini kwani ni jambo la kawaida kufanyiwa uangalizi wa kila mara .
Kibaki amekuwa na tatizo la goti tangu alipohusika katika ajali ya barabarani mwaka wa 2002 huo Machakos akifanya kampeini . Amekuwa akifanyia uangalizi na matibabu ya goti hilo tangia wakati huo .