Hapana Tambua Urembo? Tazama jinsi Polisi walivyomcharaza mwakilishi wa Mlango kubwa Patricia Mutheu

Mwakilishi wa kaunti wa Mlang Kubwa Patricia Mutheu  amejipata pabaya baada ya polisi kumshambulia kwa rungu na makonde katika jengo la city hall .

Patricia alikuwa miongoni mwa wawakilishi wa kaunti waliokuwa wameenda City Hall kumpa spika wa bunge  la kaunti Beatrice Elachi notisi ya kutaka kumfurusha afisini .

Baada ya wawakilishi wenzake kufurushwa kutoka jengo hilo , Mutheu alijipata pekee yake na polisi hawakumsaza kwani walimshambulia na kumpa kipigo  kibaya .