Kifo hakina huruma! Familia ya Diamond yaomboleza

Familia ya msanii wa bongo Diamond inaomboleza kifo cha babu yake aliyeaga dunia. Mzee Shamte ni baba yake baba wa kambo wa Diamond.

Habari za kifo chake zilitangazwa na Rally Jones kwenye mitandao ya kijamii.

Rally alikuwa na haya ya kusema mitandaoni kuhusu kifo cha babu ya msanii huyo.

“4 MAY 2020. MZEE SHAMTE BABA YANGU MZAZI 🙏.”

Mama Dangote pia naye hakuwachwa nyuma aliandika habari hizo kwenye mitandao ya kijamii. Mola awape nguvu wakati huu mgumu wanapopitia kama familia.

Kuna uwezekano kuwa mzee Shamte atazikwa hii leo jioni. Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.