Kifungo cha maisha! Mwanamke aliyemuua mumewe afungwa maisha

unnamed (2)
unnamed (2)
Mwanamke aliyemuua mumewe kwa kumkata kichwa na kurusha baadhi ya sehemu za mwili wake mtoni Nairobi amefungwa kifungo cha maisha gerezani baada ya ombi lake la kutaka awachiliwe kugonga mwamba.

Damaris Mueni Musau alishtakiwa kwa madai ya kutekeleza uovu huo kwa mwendazake Raphael Mutheka Nzembu kati ya Disema19 na 24 mwaka 2014 mtaani Buruburu.

Majaji wa mahakama ya rufaa Martha Koome, Roselyn Nambuye na Sankala Ole Kantai walisema hawakupata sababu za kutosha  kubatilisha uamuzi wa awali.

“We find no merit in this appeal. It is hereby dismissed,”  uamuzi uliofanywa na majaji hao watatu.

Maafisa wa polisi walipata begi mbili katika eneo la tukio na kupata baadhi ya sehemu za mwili wa binadamu zikiwa ndani ya begi hizo.

Mhariri: Davis Ojiambo