"Kijana alienda kunianika katika Facebook Kilimani Mums..." Mamake Lucy Wangui

WhatsApp_Image_2019_11_19_at_1.08.28_PM__1574170496_86311
WhatsApp_Image_2019_11_19_at_1.08.28_PM__1574170496_86311
Mamake Lucy Wangui amefungukia Bustani la Massawe jinsi mme wa binti wake alimtusi katika mitandao ya kijamii.

Ameyasema haya katika mahojiano na kituo hiki.

"Kijana alienda kunianika katika Facebook Kilimani Mums..."

Mama huyu alikuwa ameandamana na bintiye Lucy.

Picha za Lucy zilisambaa katika mitandao ya kijamii baada ya kudhalilishwa na kupigwa kinyama na mumewe Ken.

Kichapo hiki cha kinyama kilifanyika Jumamosi ya tarehe 9 mwaka huu.

Lucy amesema mumewe alimtwanga kwa saa moja huku amewasha sauti ya redio juu zaidi ili majirani wasiskie.

"Aliniga kwa muda wa saa moja hadi nikazirai. Alikuwa amefunga mlango kwa kufuli..."

Wiki moja na nusu imeisha tangu kisa hiki kifanyike.

Bwanake alipenda kumchapa akitoka kazi kama amechelewa.

"Aliponipiga akaona damu inavuja akaacha na akatoka. Akiniona na nywele alikuwa anaivuta na kuninyoa..."