Kijana mmoja adungwa kisu mara kadhaa katika mzozo wa shilingi kumi

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya upili ya Ivakale huko Shinyalu, amelazwa katika hospitali kuu ya Kakamega baada ya kudungwa kisu na rafikiye wa kidato cha tatu, kufuatia mzozo wa shilingi kumi

Ni kisa kilichotokea mtaa wa kambi ya mwanza Malava na polisi tayari wanamzuilia mshukiwa

huyu mtoto vile alienda kumuuliza ten bob akamwambia ndio lakini ukuje jioni. Vile alienda jioni, akamwambia simama hapa akaenda kwa nyumba akachukuwa kisu akamdunga, na tumbo ikatoka,

Mshuhudia mwaingine alisema kuhusu hicho kifo

Tumekasirika kitendo hicho kutendeka maana watoto hawa wamekuwa kama marafiki na sasa wamefika mahali wameanza kudunganan visu sio mzuri sababu ya shilingi kumi kuuwa mtu na kumaliza maisha ya mtu mwingine. Nime kasirika sana.

Kwingineko ni kuwa

Familia moja kutoka kijiji cha malimili huko Shinyalu kaunti ya Kakamega inaitaka serikali kuchunguza na kuwachukulia hatua maafisa wa polisi ambao wanasemekana kumuua kwa kumpiga risasi kijana mmoja alipokuwa akitoka kutumbuiza nyimbo za injili kwenye matanga.

Inasemekana kijana huyo Stanley Mavia alikuwa akitoka kwa matanga mwendo wa saa tisa alfajiri alipokumbana na mauti.

Hata hivyo kamanda wa polisi eneo la magharibi Wilkister Nayiyo amekanusha madai hayo akisema ni wahalifu waliohusika na mauaji hayo japo ameahidi kuendesha uchunguzi.