Kijiji cha Moi huko Baringo chakumbwa na maporomoko ya ardhi

Maporomoko
Maporomoko
Maporomoko ya ardhi yamekumba  eneo la baringo ya kati  kikiwemo katika kijiji cha Sacho cha rais wa zamani Daniel Moi .

Vijiji vingine ambavyo vimeathiriwa na mkasa huo  ni  Kiptagich, Kaptich, Kabarak, Timboiwo, Kabasis na  Tandui.  Zaidi ya familia 200 zimeachwa bila makao baada ya maporomoko hayo kuanza siku ya jumatatu na kuendeleahadi jumatano usiku .

Maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa inayoshuhudiwa katika eneo hilo  ambayo ilianza mwezi Aprili na idara ya utabiri a hali ya anga imesem mvua itaendelea hadi disemba . Naibu wa chifu wa  Kipatagich Luka Tingos  amezirai serikali za kaunti na kuu kuwasaidia wenyeji  kwa kuwahamisha hadi maeneo salama .

Kando na kuachwa bila makao ,waathiriwa wengi pia walipoteza mazao yao shambani yenye thamani ya mamilioni ya pesa  .

Kuna hofu kwamba huenda maporomoko Zaidi yakatokea hivi karibuni baada ya mipasuku kuonekana katika ardhi . Mwathiriwa Felix Cheruiyot  amesema alikuwa ndani ya nyumba na familia yake  aliposikia mlio mkubwa na mwanzoni alifikiri ni ajali ya barabarani lakini muda mfupi baadaye tope kubwa liliisomba nyumba yake .Amesema aliihamisha familia yake hadi katika  boma la jamaa yao katika kijiji jirani .

Naibu wa gavana  Jacob Chepkwony  amesema amelipa kundi moja la wataalam ka kazi ya kutathmini  hali .