Kila la heri! Raila Odinga atembelea Harambee Stars kabla ya AFCON

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga aliwatembelea Harambee stars huko Cairo Misri, na kuwahimiza wapeperushe bendera ya Kenya vyema ugenini na kuonyesha uweledi wetu katika mchezo huo.

Odinga alikua pamoja na waziri wa  Ugatuzi Eugene Wamalwa, na balozi wa Kenya nchini Misri Joff Otieno.  Raila anatarajia kutazama mechi ya Kenya ya kwanza dhidi ya Algeria Jumapili Juni tarehe 30 June Stadium pamoja na waziri wa spoti, Amina Mohamed ambaye anatarajiwa kufika huko leo.

Kenya iko katika kundi C pamoja na Algeria, Senegal na majirani wetu Tanzania.

Kipute cha ubingwa bara Afrika, AFCON kinang'oa nanga hii leo huku wenyeji misri wakikabana koo na Zimbabwe. Misri al maarufu the pharaohs, wakiongozwa na mshambulizi matata wa Liverpoool, Mo Salah wana rekodi ya mataji saba na watakuwa wananuia kuongeza la nane baada ya kunyukwa katika fainali ya mwaka 2017 na Cameroon.

Mtangazaji wetu, Fred Arocho ambaye yuko Uholanzi, anatarajia kujiunga na kikosi cha Harambee Stars hii leo.