KILGORIS: Wanne Wafikishwa Mahakamani Kwa Kuwa Na Pembe Za Ndovu

picha: the-star.co.ke | 

Washukiwa wanne waliopatikana na pembe mbili za ndovu wameachiliwa kwa dhamana ya KES 1 000 000 na mahakama ya Kilgoris.

Wanne hao walifikishwa mbele ya hakimu mkaazi Rachel Kihara Jumanne asubuhi wakikabiliwa na shtaka la kuwa na pembe mbili za ndovu zenye thamani ya KES 2 500 000 katika eneo la Olomotonyi.

Washukiwa hao, Raphael Opiyo, George Omuga, Solomon Viego na Jackson Omuga, walikanusha mashtaka hayo na kesi yao itajwa tarehe 8 Januari 2016 kabla ya kusikizwa tarehe 5 Machi 2016.

Kwa taarifa kamili, soma: