mwili wa Mildred Odira

Kilicho sababisha kifo cha mfanyakazi wa nation media Mildred

Baada ya Mildred kutoka nyumbani kuelekea hospitali aliweza kupotea kwa siku kadhaa kisha kupatikana katika chumba cha kuifadhi mati cha mji.

Mildred aliweza kuuwawa eneo lingine na mwili wake kuja kutupwa eneo la GSU katika barabara kuu ya Thika.

Upasuaji ambao ulifanywa jana ulionyeshwa kuwa Odira alikuwa na majeraha kiwiliwili. Daktari wa serikali wa upasuaji Johansen Oduor alisema kuwa Mildred aliweza kuumizwa na kitu butu, na kuaga dunia kama nyundo.

Mtoto wangu alipakwa busaa kwa kichwa na kuonjeshwa chang’aa

Jeraha ambalo liliacha shimo la centimita 2 katika paji la uso wake. Mildred, 32,alikuwa mfanyakazi wa nation media group katika kaunti ya Nairobi.

mildred odira
                  Mwendazake Mildred Odira

Viungo vyake vya ndani vilikuwa vimeharibiwa, na hakukuwa na majeraha yoyote ya kuonyesha kuwa alihusika katika ajali ya barabara.

Oduor hakuzungumza na wanahabari bali aliweza kuwaambia kwa ufupi jamaa za Mildred habari za upasuaji. Mbunge wa Suba North Millie Odhiambo akiongea kwa niaba ya familia alisema wachunguzi walichukua sampuli za DNA ili kufanya uchunguzi zaidi.

“Inakaa kuwa aligongwa na kitu butu kama nyundo kisha kuwekwa barabarani ili ionekane ni kama ajali aliofanya.” Alizungumza Millie.

Sifuna to Murkomen: We won’t hear the appeal on Aisha, Dori

Pia wachunguzi walichukua sampuli ili kufanya uchunguzi kama Mildred alikuwa amebakwa.

“Wameweza kuchukua sampuli za kucha ili kuchunguza kama marehemu huyo aliweza kupigana vita na washambuliaji hao,” Aliongeza Odhiambo.

Mwili wa marehemu uliweza kupatikana katika chumba cha kuifadhi maiti baada ya kuripotiwa kupotea Jumanne wiki iliyopita. Mwili wake ulipelekwa jana katika chumba cha kuifadhi maiti cha Lee.

Polisi walipata mwili wake kando ya barabara na kuuchukua na kuupeleka katika chumba cha mji cha kuifadhi maiti baada ya muda mchache.

Show us what your mama gave you! Millicent Omanga’s dance moves wows Kenyans (VIDEO)

Dereva aliyempeleka Mildred hospitalini, Davies Ochieng, yumo mikononi mwa polisi na kuwekwa rumande hadi Februari 14 kwa maana ni yeye muhusika mkuu katika mauwaji ya Mildred.

Familia na jamaa wa marehemu walisema kuwa Mildred aliuwawa ilhali si ajali kama ilivyosemekana awali.

Ndugu wa marehemu Carrington Ogweno alidai kuwa alipokea vitisho vya maisha kuhusiana na uchunguzi wa dadake, aliambia wanahabari kuwa wanaume wawili walimfuata mpaka nyumbani, na kumpa onyo kuwa awachane na kesi ya dadake ama pia yeye atakufa kama dadake alivyokufa.

Ogweno aliweza kuripoti katika kituo cha polisi cha Tassia na kupewa OB 02/05/2/2019. nakusema kuwa haogopi kifo.

“si tishiki wala kuingiwa na uoga kama kesi ya Mildred itanishusha chini na kuniua bora ukweli uweze kujulikana,”Alieleza Ogweno.

Ina maana kuwa waliomuuwa Mildred wanamjua mzuri na sababu wa kumuuwa ilikuwa ipi?

 

Photo Credits: the star

Read More:

Comments

comments