Kilio cha haki! Afungwa miaka 20 kwa kumnajisi msichana wa miaka 13

raila
raila
Janadume katika vitongoji vya Kitale kaunti ya Trans Nzoia  limefungwa miaka 20 gerezani baada ya kumnajisi msichana wa miaka 13 kwenye shamba la ngano.

Joseph Marani Wanyonyi alikumbana na makosa hayo baada ya mahakama kumpata na makosa ya kutekeleza unyama huo mnamo Desemba 2014.

Katika mahakama hiyo, mwathiriwa huyo ambaye anasoma katika darasa la 4, alisema kuwa alikuwa ameenda kutafuta ngano kwa shamba hilo kabla ya kufanyiwa uovu huo.

Aliongeza kuwa Wanyonyi alimsongea na kumshauri amfuate hadi upande mwingine wa shamba hilo ambapo kulikuwa na kichaka kikubwa na kumdanganya kuwa atampa ngano nyingi kando na ile aliyokuwa anaitafuta.

Marafiki wake wa karibu walihoji kuwa Wanyonyi alimdanganya mwathiriwa na kumlazimisha kutekeleza kitendo hicho cha unyama.

Akitoa uamuzi huo, jaji wa mahakama kuu ya Kitale Hillary Chemitei alisema mahakama ilimpata  mshtakiwa na makosa na hivyo atatumika kama kielelezo kwa watu wengine wanaotazamia kutekeleza kitendo kama hicho.

“This appeal is not meritorious. The trial court's findings were both sound in law and fact. The appeal is disallowed,” judge Hillary Chemitei ruled.