Kilio cha magavana! Oparanya aitaka serikali kutoa fedha za kukabiliana na corona

Baraza kuu la magavana kupitia kwa mwenyekiti wao Wycliffe Oparanya sasa wanaitaka serikali serikali kutoa mgao wa fedha walizoambiwa ili kukabiliana na virusi vya corona ambavyo vimeathiri kaunti 34 nchini kufikia sasa nchini.

Akihutubu wakati wa maadhimisho ya Madaraka jijini Nairobi,Oparanya amesema baadhi ya majimbo nchini huenda yakashindwa kukabiliana na virusi hivyo iwapo serikali haitatao pesa hizo mapema.

"Through your directive your excellency, County governments were allocated Sh 5 billion to support and complement your efforts in fighting Covid-19 pandemic," Oparanya amesema.

Oparanya ameongeza kuwa kupitia baraza hilo la magavana nchini, wametuma shilingi bilioni 6.1 katika kamati kuu ya kukabiliana na virusi hivyo.

Ameongezea kuwa hakuna mkenya yeyote katika majimbo yote 47 nchini ambaye atafariki kutokana na njaa.

"No Kenyan will die of hunger and county governments are working with Agriculture Ministry towards ensuring that," amesema Oparanya