Kilio cha Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini asema huenda maambukizi yataongezeka kwa taifa lake

Likiwa ndilo taifa la katika bara la Afrika ambalo kufikia sasa limeandikisha visa vingi vya maambukizi ya virusi vya corona takriban 22,000.Rais wa taifa hilo Cyril Ramaphosa anahofu kuwa japo wameanza kupunguza vigezo walivyokuwa wamewekea wananchi wake siku za hivi karibuni,huenda idadi ya maambukizi ikaongezeka zaidi .

Ramaphosa amesema haya baada ya kampuni ya kuchimba madini katika mji mkuu swa Johannesbaurg kusema wafanyakazi wake 164 walikuwa wamepatikabna na virusi hivyo.

Kufikia sasa Afrika Kusini ina watu 429 waliofariki  dhidi ya virusi hivyo.

Kafya iliyokuwa imewekwa kwa taifa hiloi sasa iliondolewa na kufunguliwa kwa biashara zote ili kufufua uchumi wa taifa hilo uliodorora kutokana na janga la corona.

Uuzaji wa vileo uliokuwa umesitishwa pia unatarajia kurejelea shughuli zake za kawaida baada ya taifa hilo kuongezea vigwazo vya watu kutotangamana maeneo ya vilabu.

Licha ya kukubali kufunguliwa kwa shughuli katika taifa lake,Ramaphosa amewaonya watu wa Afrika Kusini kuwa huenda maangamizi zaidi yapo njiani yaja.

“We should expect that these numbers will rise even further and even faster,” alisema Cyril.