Uchunguzi uliofanywa na Declassified UK, Daily Merverick nchini Afrika Kusini na The Star umeonyesha jinsi kikosi hicho cha siri ambacho kinalipwa na kusaidiwa na CIA kimekuwa kikiwasaka washukiwa wa ugaidi tangu mwaka wa 2004 .
Shirika la ujasusi la Uingereza MI6 pia lina wajibu mkubwa wa kuwatambua washukiwa hao ambao hukamatwa au kuuawa n na pia kufichua maficho yao .
Uchunguzio huo umebaini kwamba kikosi hicho hutumia njia a kisiri katika oparesheniu zake ikiwemo kutumia nambari feki za usajili wa magari au kuifanya kuwa wafanyikazi wa kutoa misaada katika oparesheni zinazofanyika kwenye kambi za wakimbizi.
Makomando hao ambao huvamia makaazi ya washukiwa wa ugaidi wanatoka kikosi cha Rapid Response Team (RRT), ,kundi maalum la maafisa wa skari kutoka GSU Recce Company. Kikosi cha RRT kiliundwa ,kupewa silaha na kupewa mafunzo ya kufanya oparesheni za kukabiliana na magaidi kwenye oparesheni inayoonekana kufadhiliwa na SHhirika la ujasusi la Amerika CIA ,uchunguzi ambao siri zake zimefichuliwa umonyesha
Kundi hilo la Kenya linafahamika kwa njia isio rasmi kama Rendition Operations Team na lina makomando takriban 60
Programu huyo ya siri ya CIA iliyoanza mwaka 2004 inaendeshwa na afisa mwandamaizi katika ubalozi wa Amerika jijini Nairobi lakini hadi sasa mpango wenyewe haujaangaziwa hasa machoni pa umma .
Kwa mujibu wa mahojiano na maafisa kadhaa wa CIA ,Idara ya masua ya kigeni ya marekai na maafisa wa ujasusi wa Kenya ,polisi na baadhi ya wanachama wa kikosi hicho imebainika kwamba tangu kuanzishwa ,kundi hilo limehusika kuwakamata washukiwa sugu wa kigaidi na kufanikisha oparesheni za kuwakata wengine huku baadhi ya washukiwa hao wakiuawa .