logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Misri yatokomeza ugonjwa wa malaria - Shirika la Afya Duniani

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limethibitisha kwamba Misri haina malaria

image
na BBC NEWS

Kimataifa21 October 2024 - 10:56

Muhtasari


  • "Malaria ni ya zamani kama ustaarabu wa Misri yenyewe, lakini ugonjwa ambao uliwasumbua mafarao sasa ni historia,"  Tedros alisema.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limethibitisha kwamba Misri haina malaria - jambo ambalo shirika la afya ya umma la Umoja wa Mataifa lilisema ni "la kihistoria".

"Malaria ni ya zamani kama ustaarabu wa Misri yenyewe, lakini ugonjwa ambao uliwasumbua mafarao sasa ni historia," mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema.

Mamlaka ya Misri ilizindua juhudi zao za kwanza kukomesha ugonjwa hatari wa kuambukiza unaoenezwa na mbu karibu miaka 100.

Uidhinishaji hutolewa wakati nchi inapothibitisha kuwa mkondo wa usambazaji umekatizwa kwa angalau miaka mitatu mfululizo iliyopita.

Malaria huua watu wasiopungua 600,000 kila mwaka, karibu wote ni kutoka barani Afrika.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved