Kimosop kushikwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA)

Kimosop alishikwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) siku ya Ijumaa, Julai 26, asubuhi baada ya kurudi kutoka Tanzania.

Kukamatwa kwake kulithibitishwa na wapelelezi wa DCI ambao walisema kuwa mtuhumiwa alikuwa bado anadhuiliwa na polisi kwani anasubiri kufikishwa kortini.

"David Kipchumba Kimosop, alikamatwa mapema leo kwenye uwanja wa JKIA alipofika kutoka Tanzania kwa madai ya kwa tuhuma za rushwa, sasa amedhuiliwa na polisi na anasubiri kwenda kortini kushutumiwa," alisema DCI kupitia Twiter.

David Kipchumba Kimosop anatuhumiwa pamoja na wengine 27 wakiwemo Katibu wa zamani wa Baraza la Mawaziri la Hazina, Henry Rotich na Katibu Mkuu wake Kamau Thugge ambao walihukumiwa siku ya Jumanne, Julai 23.

Soma mengi