Kinaya siku ya Mashujaa, wakenya wafunguka

navy
navy
Tarehe ishirini mwezi wa Oktoba ni siku ambayo wakenya husherehekea mashujaa.

Shujaa ni mtu yeyote yule ambaye kwa njia moja ama nyingine amechangia pakubwa kunawiri au kufaulu kwako maishani wakiwemo watu waliopigania nchi hii kupata uhuru.

Katika sherehe lililofanyika jana, hisia mbali mbali ziliibuka baada ya Rais Uhuru Kenyatta kukagua gwaride.

 Hayo yalijiri wakati wanajeshi wa kikosi cha baharini walikuwa wanaonyesha mashua zaidi ya tano wanazotumia kulinda nchi katika upande huo wa bahari.

Swali likibakia midomoni mwa wakenya je, walikuwa wapi wakati Miriam na mwanawe Amanda walikuwa wakizama kule Likoni?

Wakenya hao wanasema kuwa gari ambalo Miriam na Amanda walikuwa ndani ilielea juu ya maji kwa muda karibu daka kumi na iwapo wanajeshi hao wa kikosi cha maji wangefika mahala hapo mapema, huenda lililotendeka lisingefanyika.