Kinaya:Vituko vya Wachina kutoroka Kenya wakihofia kuambukizwa Covid 19

Serikali ya  uchina imeanza kuwasafirisha raia wake 400 kutoka Kenya ili warejee nchini mwao wakihofia kuambukizwa virusi vya corona .

200 kati yao tayari wamendoka nchini huku 200 wengine wakitarajiwa kusafiri wakati wowote wiki hii .

Wakili wao Isaac Okinyo alifaulu kupata idhini ya mahakama kwa wateja wake kuondoka nchini baada ya ombil lake la hapo awali kwa wizara ya masuala ya kigeni na ubalozi wa China kukataliwa .

Wachina hao wamesema mfumo wa aafaya nchini una udhaifu mkubwa wa kuweza kukabiliana na janga la covid 19 na hivyo basi wanafaa kupewa ruhusa ya kurejea nchini mwao .