King Kaka asifu Kansoul baada ya kuachia 'Kula Vako'

King Kaka amewasifu Kansoul baada ya kutoa kibao kipya 'Kula Vako'. Kibao hicho kilichotolewa wiki iliopita ni kolabo baina ya King Kaka na wakali hao wa Kansoul huku kikiwa kimeelekezwa na Ricky Bekko. Mejja,Kid Kora pamoja na Madtraxx ndio wanao unda kundi la Kansoul .

Tangu kuachiliwa kwake, Kula vako imekuwa ikisikizwa nchini kote na hasa kwenye mtandao wa  Youtube." Mimi na Kansoul tumekuwa marafiki wa chanda na pete na jambo hilo limetuunganisha na kupelekea kuwafurahisha mashabiki kwa wakati mwingine," King Kaka alisema.

Kwa pamoja, King Kaka na Kansoul waliachilia kibao cha Ligi soo kilicho onekana na mashabiki elfu mia mbili."Kula vako maana yake ni kuichukulia hali kwa utaratibu kama umetulia. Ningetaka mashabiki na watu wote wasiwe na msisimko wowote na maisha,"Alieleza King Kaka.

?list=RDn-uuQRVedDk