Kinoti, aonya wahalifu waliotorokea nchi za kigeni

Mkurugenzi wa upelelezi nchini (DCI) George amesema kwamba mataifa ya Afrika Mashariki yanafaa kuwashughulikia wahalifu wanaoendesha uhalifu katika kanda hii.

“Tunahitaiji kuwa wakatili dhidi ya makundi haya ya kihalifu ... tutayakomesha ,” alisema.

Kinoti alikuwa akizungumza siku ya Jumanne, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaoleta pamoja wasimamzi wa mashtaka kutoka nchi za Afrika mashariki. Alisema njia ya pekee kuangamiza makundi ya kihalifu ni mataifa ya Afrika Mashariki kushirikiana ili kukabili mipango ya makundi haya.

Kinoti alisema kwamba bidhaa ghushi, ugaidi na wizi wa mabavu ni baadhi ya uhalifu unaoathiri nchi kadhaa.

Alisema bidhaa gushi na zile ambazo zimeptisha muda wa matumizi zimekuwa zikiingizwa kimagendo na kupakiwa upya katika mifuko mingine na kusambazwa masokoni.

Kinoti alitoa onyo kali kwa watu wanaoiba pesa kutoka nchi moja na kuwekeza katika nchi zingine.

“Hutawahi tena kuiba kutoka nchi moja na uishi raha mstarehe katika nchi nyingine. Tutakuzoa mafichoni.

Mkurugenzi wa mshataka ya umma Noordin Haji kwa upande wake alisema kwamba makundi ya kihalifu yalionawiri yanahitaji ushirikiano wa kimaeneo na kimataifa kuukabili.

Haji alisema kwamba sera za kitaifa, kanda na kimataifa za kukabiliana na uhalifu zinafaa kuungwa mkono ili kukabili kabisa uhalifu wa kimataifa. Ofisi ya mkurugenzi mkuu kwa umma ndio mwenyeji wa mkutano huo unaolenga kukabiliana na uhalifu wa hadhi ya juu.