Kinoti apata pigo baada ya mahakama kusema ni Haji pekee mwenye uwezo wa kufungulia mashtaka

DCI
DCI
Mkurugenzi wa idara ya mahakama hana maamlaka ya kufungulia yeyote mashtaka ila kwa idhini ya  mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma  Noordin Haji  ,mahakama imeamuru.

Hii ni baada ya kuzuka  malumbano  kati ya afisi hizo mbili  kuhusu aliye na maamlaka zaidi kuhusiana na kuwafunguliwa washukiwa mashtaka .

Jaji George Odunga  alhamisi ameamuru kwamba DPP ndiye  mwenye maamlaka ya kufungua na kumshtaki mtu. Hatua  hiyo ilijiri baada ya  mkuu wa  maamlaka ya ukusanyaji wa raslimali za maji  Geoffrey Sang  kwenda kortini akipinga kukamatwa na DCI . Sang alikamatwa mwezi Aprili  kwa kushukiwa kuhusika na sakata ya uporaji wa fedha za kujengwa mabwawa .

" DCI hana maamlaka wala uwezo wa kuanzisha mashtaka  dhidi ya mtu yeyote ila kwa idhini kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma’ jaji Odunga amesema.

Odunga  aliikosoa idara ya DCI kwa kumkamata  Sang bila waranti  .