Kinoti ataka Malala ashtakiwe kwa madai ya uongo kuhusu njama ya kumuua

Mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai George Kinoti akiwa mbele ya seneti huku akihojia alimtaka seneta wa Kakamega kukamatwa baada ya madai ya uongo ya mauaji.

Kinoti alihojiwa na seneti ili kuweka wazi kuwa maisha ya Malala yalikuwa hatarini.

Seneta huyo alidai kuwa kikundi maalum kimetengwa ili kumfuata na nia yao ili kuwa ya kumuua, hata hivyo Kinoti alisema uwa uchunguzi ulibaibi kwama madai hayo yalikuwa ya uongo na mabaya.

"Kitengo cha huduma maallum,ni kitengo katika DCI ambacho hufanya uchunguzi kwa maagizo ya mwelezi wao utafutaji wa besi za data za wafanyakazi wa DCI hazikupata jina la afisa ambaye alikuwa katika barua ya ulalamishi

hakuna afisa wa polisi ambaye anajulikana kama chifu inspekta Wanzala katika kitengo na besi ya data yote ya DCI,mapendekezo kutoka kwa uchunguzi huu ni kuwa madai hayo yanahusisha wafanyakazi wa idara ya DCI madai iliowatia kejeli na tuhuma kutoka kwa wananchi ambao wanawafanyia kazi kwa bidii

tukizingatia ushahidi ulio kwenye rekodi tumepata kadai ya seneta Malala ni ya uongo na yenye nia mbaya tunawasilisha anapaswa kushtakiwa kwa kufanya na kupeana hakikisho la uongo kinyume na sehemu (59)b ya kanuni za adhabu."Kinoti Alizungumza.