Kiongozi wa genge la wezi wa magari akamatwa ,magari 7 yapatikana

mwizi 1
mwizi 1
Mwanamme mwenye umri wa miaka 48 anayemainika kuwa kiongozi wa genge la wezi wa magari katika eneo la magharibi amekamatwa .

Davis Migosi,  mwalimu katika shule ya St Columbans Secondary School in Kitale, anashukiwa kuwa kiongozi wa genge  hilo .

Kupitia twitter ,DCI imesema  Migosi amekuwa akijificha katika eneo la Matunda tangu juni tarehe 8 wakati washirika wake walipokamatwa .

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1279170705112928257

Alikamatwa pamoja na  ; Asman Memba Bakari 38, na  Jeremiah Yego Kiptoo 34.

Mkuu wa DCI GEORGE Kinoti amesema  magari saba yalipatikana pamoja na stakabadhi 17 bandia za kumiliki magari .

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1279170862256656385

Magari mengine yalliopatikana ni Toyota Axio KCL 790N, Toyota Hilux KBB 876A,  gari jeupe la Toyota Probox  bila nambari za usajili  ,Toyota DX KBJ 316D, Toyota Premio KBN 377A, Toyota Hiace KCL 378K, Isuzu D-MAX Pick Up KCR 734T,  na nambari bandia za usajili wa magari .

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1279170799321133058