Kiongozi wa kanisa amuua rafikiye baada ya kumpata akimlipua lungula mkewe

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Kakamega sasa wameanzisha msako wa kumtafuta jamaa wa miaka 40 baada ya kuhusishwa na mauaji ya rafikiye kwa tuhuma za kushiriki ngono na mkewe.

Tukio hilo limetokea katika boma la Edmond Inzai, mkaazi wa KonaMbaya  katika eneo bunge la Lugari.

Mwathiriwa Fred Khamasi wa miaka 32 na ambaye ni kiongozi wa kanisa la African Divine Church ADC, anadaiwa kutoka nyumbani kwake usiku bila ya kumjulisha mkewe Ann Alusa.

Baadaye, mida ya saa 11 usiku, mkewe anasema bwanake alirejea nyumbani akiwa anavuja damu nyingi kutokana na kukatwakatwa kwa panga .

“Later, at around 11pm, he returned home with deep panga cuts inflicted to his head, arms and different parts of his body. Blood was gushing from the cut parts,”Alusa.

Jaribio la kumkimbiza katika kituo cha afya cha Lumakanda liliambulia patubu kwani aliaga dunia akipokea matibabu.

Asasi za usalama eneo hilo zimebaini kuwa, Khamasia alishambuliwa na Inzai baada ya kumpata akishiriki mapenzi na mkewe.

Inasemekana kuwa Inzai ambaye ni mchungaji wa kanisa la PAG katika eneo la Lugari alirejea nyumbani bil ya kumjulisha mkewe na kupata rafikiye wa dhati akiwa anamnyandua kweli kweli.

Mkuu wa polisi kaunti hiyo sasa anasema kuwa harakati za kumtafuta mshukiwa zimeanza huku mwili wa mwendazake ukiwa umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kakamega.