Kiongozi wa wengi kwenye bunge Aden Duale atangaza msimamo wake wa kisiasa

29663257_2009436795752983_9140692899263207740_o
29663257_2009436795752983_9140692899263207740_o
Hivi majuzi, rais Uhuru Kenyatta aliwatimua wandani wa naibu wake William Ruto kutoka nyadhifa zao katika seneti. Wandani wake sasa wanasema shoka lake linaelekea bungeni ambapo wote waaminifu wa Ruto watafurushwa.

Kiongozi wa wengi Aden Duale amechukua hatua ya mapema ya kutangaza msimamo wake baada ya kubadilisha picha yake kwenye ukurasa wa facebook na kuweka yake akiwa na rais Uhuru Kenyatta.

Duale ametangaza msimamo wake kisiasa na kuonyesha kuashiria kuwa yeye ni mwaminifu kisiasa kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Huku Rais akianza mikakati ya kuwakata miguu wandani wa Naibu Rais William Ruto, Duale ameonekana mjanja.

Hatua ya Duale imeonekana kama tangazo kuwa yeye anamfuata Rais Uhuru na ni mwaminifu kwake. Alifanya hivyo siku moja tu baada ya Uhuru kuwatimua kiongozi wa wengi kwenye seneti Kipchumba Murkomen na kiranja Susan Kihika.

Nduru za kuaminika zinaarifu kuwa baada ya kumalizana na seneti, sasa shoka la  Uhuru linaelekea kwenye bunge la kitaifa ambapo ananuia kufanya mabadiliko katika kamati kuu muhimu na ambazo zinashikiliwa na vibaraka wa naibu rais Ruto.

Duale ni mmoja wa wafuasi sugu wa Ruto lakini kwa sasa anaonekana amebadili njia yake na kuwa mfuasi wa rais Uhuru Kenyatta. Kwa kweli hawakukosea waliposema mwenye macho haambiwi tazama.

Kiongozi huyo ameonekana kuwa mjanja wa kupindukia, ni picha ambayo iliwafanya mashabiki wake kutoa hisia tofauti na hizi hapa baadhi za hisia hizo.

The man standing beside you is scorching your Image as good Leader. Avoid Him that we love you Aden as Mount Kenya region People

Have you changed today this profile picture bwana Duale

You've realised you were on the wrong track.

This picture says it all, you now know who is the Boss..

kama n ruto amaua vnye 2liamua n ruto bana, y do u pretend kwa hii profile,,,come out clean on social media na u2uambia umedump WSAR,,,ruto mbele 2022!!!

Mr Duale umeanza kufunguka macho but i think its too late,....acha wenye wamelalisha masikio waendelee kulalalisha