Kipchoge

Kipchoge atoa siri kuhusu mapenzi yake ya riadha

Gwiji Eliud Kipchoge ambaye anatarajiwa kuvunja rekodi yake kwenye mbio za marathon kule Austria Vienna Jumamosi, amesema kwamba kukimbia huimarisha  afya mwilini na  husaidia akili kufikiria vizuri.

“Ninapenda kukimbia kwa sababu husaidia mwili kuwa na afya njema na  kufanya akili yako ifikirie vizuri, bingwa wa dunia wa Olimpiki Eliud Kipchoge alisema.

Akijibu maswali kutoka kwa mashabiki wake, Kipchoge alisema kwamba alianza kukimbia  tangu akiwa na miaka 17 iliyopita baada ya kupewa motisha na kocha wake.

“Nilitiwa moyo na mkufunzi wangu mnamo 2003. Kuwa na subira na kujitolea ni mambo kuu yanayoniongoza na nimejifunza kama mkimbiaji,” alisema.

Nyota Eliud Kipchoge Kutimua Viena Kesho, Ineos Ina Maana Gani?

Alipoulizwa kuhusu utaratibu wa amzoezi yake kabla ya kukimbia, Kipchoge alisema kila anachofanya ni kunyoosha  viungo vya mwili wake mwanzo

“Ninafanyia mazoezi yangu nchini Kenya … kwa viatu  aina toafuti kutoka Pomelo hadi Pegasus .. hivyo ni viatu vyangu  vinavyovipenda,” Kipchoge  alisema.

Kwa Eliud Kipchoge kukimbia 1:59, anahitaji kukimbia kwa kasi ya wastani ya;

100 m kwa sekunde 17.08

200 m kwa sekunde 34.17

400 m kwa dakika 1 sekunde 8

800 m kwa dakika 2 sekunde 16

1500 m kwa dakika 4 sekunde 16

Dakika 5000 dakika 14 sekunde 13

10,000 m 28 dakika 26 sekunde 26

Nusu marathon dakika 59 sekunde 59

Marathon 1 hr dakika 59 sekunde 59

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, Kipchoge alisema anahisi yuko tayari zaidi na amejiandaa na mbio za Vienna vyema.

“Ninajiamini kwa sababu nimekuwepo hapo awali. Kilomita zote kwenye riadha ni muhimu na ninachukua umbali wote nitakimbia kuwa muhimu,”  bingwa huyu wa dunia alisema

Kipchoge Akiri Kuwa Mtulivu Kabla Ya Jaribio Lake La Ineos1:59 Challenge

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments