Kipchoge with First Lady-compressed

Kipchoge, Kenyatta wafanya mazoezi Ikulu, katika uzinduzi wa Beyond Zero

Mama wa Taifa Margaret Kenyatta alijumuika na bingwa wa olimpiki wa mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge kwenye ikulu ya Nairobi katika uzinduzi wa mbio za Beyond Zero.

Hafla ya Beyond Zero Half Marathon inatarajiwa kufanyika Machi tarehe 8, 2020 jijini Nairobi.

Moses Kuria Apuuzilia Mbali Ripoti Ya BBI, Adai Ni ‘Feki’

Katika uzinduzi huo, Mama wa taifa alidhihirisha kujitolea kimasomaso katika kutetea huduma za afya kwa watoto na wanawake kote nchini.

Aidha, Margaret Kenyatta alifanya mazoezi ya riadha katika ikulu pamoja na Eliud Kipchoge na mkewe Grace mwendo wa asubuhi.

 

kipchoge beyond zerro campaing-compressed

Mama wa taifa pia alitangaza kuongezwa kwa nafasi za watakaonufaika na ufadhili wa masomo kutoka 100 hadi 200 hapo mwakani.

Alisema kuwa fedha zitakazo changishwa katika hafla hiyo zitatumika kuimarisha vifaa vya kliniki pamoja na ujenzi wa maeneo ya kimatibabu ya Beyond zero.

Miongoni mwa waliokuwapo ni mawaziri Amina Mohammed na Margaret Kobia pamoja na Seneta Beth Mugo na  Ida Odinga mkewe kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

 

 

 

 

 

 

 

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments