Kipchoge The Great! Eliud ashinda tuzo ya SOYA ya mwanaspoti bora

Kipchoge
Kipchoge
Eliud Kipchoge,  mwanariadha bora wa mbio za marathon ndoue pia mwanaspoti bora mwaka huu  baada ya kutunikiwa taadhima hiyo katika tuzo Za SOYA .

Mshikilizi huyo wa rekodi ya dunia ya marathon  awali alikuwa ametuzwa kama mwanaspoti bora baada ya kumpiku  bingwa wa mbio za mita 1500  Timothy Cheruiyot  na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za  dunia za half marathon  Geoffrey Kamworor.

" Uhuru upo katika michezo’ amesema Kipchoge .

Gwiji wa soka wa Nigeria  Victor Ikpeba  ndiye aliyekuwa mgeni  staa katika hafla  hiyo iliyohudhuriwa pia na waziri wa spoti Amina Mohammed ,katibu wa kudumu wa wizara hiyo Joe Okudo na rais wa NOK Paul Tergat ambaye pia ndiye mwanzilishi wa tuzo ya Soya . Bingwa wa dunia katika mbio za mita 5000 Hellen Obiri ndiye alieyeshinda tuzo ya mwanaspoti bora wa kike  mwaka huu .mshililizi wa rekodi ya mbio za marathon  Brigid Kosgei  alimalia wa pili ilhali bingwa wa  marathon dunia  Ruth Chepng'etich  alimaliza wa tatu .