Kipchumba Murkomen Ahusishwa Na Njama Ya Kupeleka William Ruto Hague

Kipchumba Murkomen. | image source: standardmedia.co.ke

Shahidi mmoja wa upande wa utetezi katika kesi ya ICC dhidi ya naibu wa rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang amedai kwamba maseneta Kipchumba Murkomen, Stephen Sang na Omar Hassan walihusika na njama ya kuhakikisha kuwa naibu wa rais anafikishwa katika mahakama hiyo.

Shahidi huyo, anayetambulika kama Philip Koech amesema, maseneta hao walilisaidia shirika moja la maendeleo kuwapa mafunzo mashahidi na jinsi ya kutetea ushahidi wao wakiwa katika mahakama hiyo.

Katika habari husika, baadhi ya viongozi wa muungano wa Jubilee wameapa kupiga kambi jijini Hague tarehe 18 mwezi huu wakati wa mkutano wa mataifa wanachama wa mwafaka wa Roma.

Viongozi hao wamesema kuwa hatua hiyo inalenga kuishinikiza ICC kutupilia mbali kesi dhidi ya Ruto na Sang.