KIRINYAGA: Mwanamme Alazwa Baada Ya Kuchomwa Na Mkewe

Mafuta ya taa. | picha: indianexpress.com

Mwanamme mmoja amelazwa katika hospitali moja huko Kirinyaga baada ya kuchomwa na mkewe walipogombana kufuatia mzozo wa kinyumbani.

Inadaiwa kuwa mkewe alisubiri hadi mwathiriwa alipolala kisha akamwagia mafuta ya taa na kuwasha moto kabla ya kutoroka.

Polisi wameanzisha uchunguzi kwa kisa hicho na wanamsaka mwanamke huyo.