Kirundi & Company Advocates yatangaza siku ya kusoma wasia wa Tob Cohen

Wasia wa mwendazake Tob Cohen unatarajiwa kusomwa kesho Ijumaa.

Barua rasmi kutoka kwa kampuni ya sheria Kirundi & Company Advocates inaonyesha taarifa hizi.

Wasia wa Tob Cohen utasomwa kesho katika ofisi za kampuni hii mwendo wa saa tano unusu mchana.

Soma hapa hadithi nyingine:

Haya yanajiri baada ya mwili wa Tob kufanyiwa upasuaji.

Wasia huu unatarajiwa kuwa na maagizo kuhusu jinsi urithi wa bilionea huyu utagawanywa.

Cohen atazikwa jumatatu katika sehemu ya faragha.

Mazishi haya yanapaswa yafuate sheria na itikadi za wayahudi.

Soma hapa hadithi nyingine:

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Cliff Ombeta akiwa na Philip Murgor wametangaza kuwa mjane wa Cohen Sarah na dadake Tob watakuwepo katika hafla ya mazishi.

‘Itikadi za mazishi zitakwenda sawa na mila za wayahudi na zitaendeshwa na viongozi wanaohusika wa jamii hiyo” Amesema Ombeta.

Soma hapa hadithi nyingine:

Kwa mujibu wa Murgor na Cliff, DPP,DCI na viongozi wa idara ya mahakama wameombwa na Sarah na Gabrielle kuendesha hafla hiyo.

Mwili wa bilionea huyu ulipatikana wiki iliyopita Ijumaa baada ya kupotea kwa wiki 8.