Kisa cha Ebola Charipotiwa Kericho

Maafisa wa afya katika kaunti ya Kericho wapo katika hali ya tahadhari baada ya kuripotiwa kisa kimoja cha ugonjwa wa Ebola. Hii ni baada ya mgonjwa mmoja wa kike kuripotiwa kuwa na daalili za ugonjwa huo  katika hospitali ya rufaa ya Kericho  na baadaye kufichua kwamba alikuwa amezuru mji wa malaba ,kaunti ya  Busia katika mpaka wa Kenya na Uganda  kumwona mpenzi wake .

Awali mgonjwa huyo alilazwa katika hospitali  ya Siloam  kabla ya kuhamishwa hadi katika hospitali ya rufaa ya Kericho.Siloam  imesema ilimhamisha mgonjwa huyo ili kuafikia matakwa ya arifa kutoka wizara ya afya inayowahitaji wahudumu wote wa afya  kuripoti visa vya daalili za Ebola mara moja .

Ugonjwa huo umetokea DRC hadi Uganda ambako watu wawili wamethibitishwa kuaga dunia  waliposafiri kwenda DRC kwa maaazishi ya jamaa yao.