Kisumu: Jamaa Asakwa Na Polisi Kwa Kumnyanyasa Mtoto Wa Kambo

childabusevictim
childabusevictim
Maafisa wa polisi jijini Kisumu wanamsaka jamaa mmoja mwenye umri wa makamo, amabaye anakisiwa kumpiga na kudaiwa kujaribu kumchoma mtoto wake wa kambo katika eneo la kotur, jimbo la kisumu.
Inadaiwa kuwa Nimrod Nyongesa alimfungia mtoto huyo mvuluna mwenye umri wa kati ya miaka miwili na mitatu kwenye nyumba, na kisha kuwasha moto, na kudai kuwa mtoto huyo alikua amemwaga mchanga kwenye unga.
Mamake mtoto huyo alikua amekwenda kazini huku ikiwalazimu majirani kunvunja mlango wa chumba hicho, ili kumuokoa na kuuzima moto huo.
Majirani walichukua hatua hiyo baada ya kuona moshi ukifuka kutoka chumba cha mshukiwa.
Huyu hapa jirani aliyesababisha kuokolewa kwa mtoto huyo.