Kiswahili Kitukuzwe; Beyonce azindua kibao kipya kwa kiswahili

Mwanamziki maarufu nchini Marekani, Beyonce amezindua kibao kipya chenye mshororo wa lugha ya kiswahili ndani yake. Lugha ya kiswahili inayojulikana sana maeneo ya Africa mashariki imekua ikienea kwa kasi ulimwenguni.

"Uishi kwa Muda mrefu mfalme," mshororo aliotumia Beyonce kwenye wimbo wake huo mpya. Mshororo huu unaoanza wimbo huo.

Beyonce kwenye kibao hicho kipya kinachohusiana na filamu ya Lion King amehusisha Lugha ya kiswahili ndani yake huku akionesha jinsi anavyoipenda lugha ya kiswahili.Filamu ya Lion King inatarajiwa kuonyeshwa tarehe kumi na tisa mwezi huu.

Kampuni ya Disney imetangaza kuwa wimbo huo mpya wake beyonce ndio  utakao tumika ndani ya filamu hio. Kiswahili kitukuzwe.