Kitendawili cha zidi kuwa kigumu zaidi,' Upasuaji bado kubaini kilichosababisha vifo vya watoto wawili Athi river

Ni kitendawili ambacho kinazidi kuwa kigumu kila kuchao, huku wengi wakingoja matokeo ya nini haswa kilichosababisha kifo cha Alvina Mutheu, 3, na Henry Jacktone, 4.

Upasuaji uliofanywa na daktari wa watoto Johansen Oduor kwa mauaji ya wawili hao ulitokea kama hauko sawa.

Kulingana na Oduor, upasuaji huo haungebaini kiini cha mauaji hayo kwa maana miili ya watoto hao wawili ilikuwa imeoza kupita kiasi.

Mili ya Alvina Mutheu na Henry Jacktone ilipaikana katika gari moja lililokuwa  limeegeshwa katika kituo cha polisi cha Athi River wiki jana.

Oduor pia alisema kuwa hakukuwa na majeraha yoyote au mifupa iliyovunjika ili kubaini kuwa watoto hao waling'ang'ana walipokuwa wanauliwa.

Madkatari wa serikali wamepokea sampuli za mili hiyo kwa utafiti zaidi ili kubaini ni nini haswa kilichosababisha vifo vya wawili hao.

Alvina na Jacktone walipotea mnamo Juni, 11, huku wasijulikane walikoenda, huku kwa njia tatanishi wawili hao walipatikana katika kituo cha polisi walikoenda kuripoti kupotea kwao.

Ripoti pia ilionyesha kuwa wawili hao walionekana wakiwa hapo huku wakitembea kuelekea katika kituo cha polisi cha Athi-river, mwanabiashara mmoja katika eneo la polisi alisema kuwa aliwaona wawili hao mwendo wa saa tano asubuhi ilhali hakuwaona tena wakitoka kwenye kituo hicho.

Je, nani alitekeleza kitendo hicho na kuwauwa wawili hao wasiokuwa na hatia na haswa kwa nini alitekeleza kitendo hicho na kwa nini hakuwa na moyo wa huruma alipokuwa akiwaua? Ni maswali ambayo wengi wamejiuliza yasiyo na majibu.