Out: Kithure Kindiki apoteza kiti cha naibu spika wa senate

Ruto 2
Ruto 2
Naibu spika wa senate Kindiki Kithure amekipoteza kiti hicho baada ya maseneta kupiga kura ya kumfurusha.

Katika majadala uliodumu kwa saa nne, maseneta 54 walipiga kura ya kumuondoa kindiki kutoka kiti hicho. Waliopinga hoja hiyo ni maseneta  saba.

Spika Ken Lusaka  aliaziacha nje  kura mbili za  maseneta waliotaka kupiga kura bila kuwepo  baada ya kiranja wa walio wengi Irungu Kang’ata kumshauri kufanya hivyo ili kuepuka  pingamizi zozote. Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen  alikuwa amepinga kuongezwa kwa kura hizo mbili  akisema ni ukiukaji wa katiba.

Awali Kindiki  alionyesha masikitiko kwamba chama  chake cha Jubilee kilikuwa kikijadili hoja ya kumuondoa ilhali taifa linakabiliwa na changamoto nyingi  likiwemo janga la  virusi vya corona, hali mbaya ya uchumi  na uvamizi wa nzige.

Alisema ni jambo la kusikitisha kwamba anashtumiwa kwa kutomheshimu kiongozi wa chama cha Jubilee rais Uhuru Kenyatta  ilhali ana heshima kubwa sana kwa rais.

Amesema wanaomhujumu sio rais Kenyatta wala maseneta.