Kizaazaa baada ya maiti kukataa kuzikwa Malindi

Kisa cha malimwengu na cha kutisha kilisimuliwa na mtangazaji Ghost asubuhi ya leo katika kipindi cha Patanisho. Alidokeza kisa na ambapo mwili wa mwenda zake Kabunda kutoka kitongojiduni cha Mnazi Mrefu  kilichopo kaunti ya Malindi kilizua hali ya wasiwasi katika hafla ya kumpa heshima mwendazake.

Mwili ulisafirishwa kutoka chumba cha kuhifadhi maiti na watu walikuwa tayari kumzika mzee huyu .Mipango yote ilikuwa ishafanyika na watu kutoka tabaka mbalimbali walikuwa wamefika kumzika marehemu.

Mzee huyu alikuwa kabla aiage dunia ametangaza kuwa dadake ambaye ni pacha wa mzee huyu lazima ahusishwe katika kupanga mazishi. Jamaa na marafiki kwa sababu zisizoeleweka walimtenga dada huyu na kukosa kutii amri za mwendazake.

Kizaazaa kilitokea wakati kuta za kaburi zilianza kubana jeneza pindi tu lilipoanza kuteremshwa. Sanduku la mzee wetu  lilipasuka na mwili wa maiti pamoja na suti yake kuanguka nje na kutapakaa.

Soma mengi hapa:

Watu walipigwa na butwaa sana na kizungumkuti hiki na wakataka kujua kilichofanya marehemu kukataa kuzikwa. Wanafamilia walidokeza kuwa walikiuka mila za wafu na itikadi za mwendazake. Waifunguka na kusema kwamba ili mazishi yaweze kuendelea lazima dadake awepo .Dadake aliweza kuitwa na mazishi yakaendelea vizuri bila matatizo.