Kizaazaa: Hotuba ya waziri mkuu wa Lesotho yapotea, Uhuru acheza densi

Waziri mkuu wa Lesotho
Waziri mkuu wa Lesotho
Waziri mkuu wa Lesotho Motsoahae Thomas Thabane yupo nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu.

Muda mfupi tu baada ya kukaribishwa na rais Uhuru kuhutubia wanahabari, Thomas Thabane ambaye alikuwa akisimama karibu naye kwenye mkono wa kushoto alishtuka kuwa hakuwa na hotuba yake iliyoandikwa.

Hapo ndipo aliwatazama wajumbe wake na kuwauliza hotuba yake.

"Karatasi yangu iko wapi ? Hakuna hapa?" alisema. Pia alisikika akimwambia Uhuru, " Sina karatasi yangu ya hotuba."

Baada ya mtafaruku huo, kicheko kilishuhudiwa kutoka hadhira ilyokuwa tayari kusikiza ujumbe wake.

Thabane hakuzungumza kwa zaidi ya dakika tano.

Katika hafla hiyo, Kenya iliomba Lesotho kuunga mkono juhudi zake za kupata uanachama usio wa kudumu katika shirika la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Naye waziri mkuu aliahidi kupigia Kenya upao katika juhudi hizo.

"Kuidhinisha Kenya katika muungano wa Afrika kama mwanachama asiye wa kudumu katika baraza la usalama kwenye umoja wa mataifa katika kipindi cha 2021-2022 ni ishara tosha kwamba ushirikiano muhimu upo baina ya mataifa haya mawili," Uhuru alisema.

Thabane hakusita kumshukuru Uhuru kwa kuwa 'rafiki mwema na karimu.'

Lakini muda mfupi tu baada ya taarifa hiyo kwa wanahabari, Uhuru alimsindikiza mgeni wake hadi kwa gari lake na baada ya kumuaga, rais alizungumza na makatibu wa masuala za kigeni Kamau Macharia na Ababu Namwamba.

Akiwa mchangamfu, Uhuru akiondoka afisini alionekana akipiga makofi huku akicheza densi kabla ya kuzungumza na katibu wake wa kibinafsi.

Katika mkutano uliodumu kwa masaa matatu, rais wa Kenya na Lesotho walitia saini mkataba wa maafikiano