Kizaazaa kanisani baada ya vijana kuchukua mwili wa mwanamke

rsz_dsc_0273-e1495457159638
rsz_dsc_0273-e1495457159638

Kizazaa kilishuhudiwa katika kanisa la overcoming faith mjini kakamega.

Hii ni baaada ya kundi la vijana waliokuwa wamejihami kuingia kanisani na kuuchukua mwili wa mwanamke mmoja kuzuia pendekezo la kumpeleka kwa bwanake mdogo.

Inadaiwa vijana hao walikuwa wametumwa na watoto wa marehemu aliowazaa katika ndoa yake ya kwanza eneo la bukhaywa ambao walipinga hatua ya kupelekwa kwa bwanake mdogo baada ya ibada.

"Tulikuwa tumeelewana mwili tutoe katika chumba cha kuifadhi maiti leo, tupeleke kanisani baada ya kanisani tumpeleke alipokuwa anaishi kisha tulale.

Alhamisi tuondoe mwili tukienda kumzika kwa watoto wake wakubwa,"Alisema mmoja wa washiriki.

Inasemakana kuwa vijana hao walikuwa wamejihami na rungu ili waweze kupiga wakristo wa hilo kanisa.

Waliweza kungoja askofu kumaliza kuomba kisha wakachukua mwili wa marehemu wakaenda kisha wakakimbia kuupeleka kwa mume wake wake.

Waliongezea kuwa watu wa kijiji hicho hawana shida na wao pia marehemu aliweza kuishi na mume wake kuanzia mwaka wa 1976.

Walidai kuwa mume wa marehemu hana ameumia miguu na hata hajaweza kuona mwili wa marehemu tangu afariki.