Kizaazaa! Wawakilisha wadi kaunti ya Kisumu walishana makonde

51078401_775767529462677_193367920574081424_n(2)
51078401_775767529462677_193367920574081424_n(2)
Kizaazaa kilishuhudiwa katika bunge la kaunti ya Kisumu pale wawakilishi wadi walipoanza kulishana makonde kulalamikia kutimuliwa kwa mwenyekiti wa bajeti Steve Owiti.

Pia ni mwakilishi wadi ya Kolwe Mashariki wakisema hatua hiyo iliendeshwa kinyume na taratibu zinazohitajika.

Kisa hicho kilitendeka baada ya wawakilishi wadi kurushiana Makonde kufuatia kutimuliwa kwa mwenyekiti wa bajeti  na ambaye pia ni mwakilishi wadi ya Kolwe east Steve Owiti katika wadhifa huo bila kufuata taratibu mwafaka.

Kwenye vurumai hizo, wawakilishi wadi wameshtumu jinsi spika wa bunge hilo Onyango Oloo alivyoongoza  shughuli ya kumuapisha mwakilishi wadi ya North Kisumu Judy Ogada kuchukua nafasi hiyo, hatua ambayo kiongozi wa walio wengi bungeni Kenneth Onyango amepinga akisema haikufuata utaratibu unaohitajika.

"Tuliweza kupata katika karatasi ya amri kua Judy alikuwa anataka kuapishwa, mwakilishi huyo wa wadi anaapishwa bila ya sisi kupiga kura,

"Na pia kuapishwa kama mwakilishi Steve hajapewa nafasi ya kujitetea na kunasikia kuwa utaratibu huo wa kumuapisha haujazingatia katiba wala kufuata utaratibu unaofaa," Alieleza Onyango.

Aidha, Owiti alimshtumu spika Oloo akisema ndiye aliyepanga kutokea kwa purukushani hizo na ameapa kutobanduka kutoka kwenye wadhifa huo, huku akiahidi kuelekea mahakamani kutetea nafasi yake.

"Spika ndio amefanya vurugu hivi kutokea na ilikuwa imethibitishwa moja kwa moja," Alizungumza Owiti.

Amehoji kuwa, kuondolewa kwake kwenye wadhifa huo kumechochewa kufuatia hatua yake ya kukataa kutenga shilingi milioni 200 kufadhili ujenzi wa makaazi ya spika na milioni 400 za ujenzi wa jengo  jipya  la bunge hilo.

"Ni ukweli kuwa mambo mengi ambayo tulikuwa tunataka na ninasema tena mambo hayo hatuwezi timiza na millioni 200,haya ni mambo ambayo yamesababisha purukushani hizi,"Alieleza Owiti.