Kizazaa Kanisani Baada Ya Mhudumu Wa Klabu Kulalamikia Kutolipwa Na Mhubiri

Basi kama ilivyo ada ya mtangazaji wa kipindi cha asubuhi cha Gidi na Ghost Asubuhi, Ghost alivuka mwaka wa 2017 na uchangamfu si haba.

Kama kawaida hakuwacha ucheshi wake mwaka wa 2016 na basi juzi alisimulia kisa kimoja cha kuchesha ambapo mhubiri aliwachwa mwenye aibu tele baada ya mhudumu wa klabu kudai kuwa mtumishi ule wa mungu alidinda kumlipa fedha alizokuwa amemkopesha hapo awali.

Basi mwanadada yule alipogundua maji yamezidi unga aliamua kufa kupona na kuzua vurugu kanisani mwa jamaa ule huku akidai waumini hawatatoa sadaka iwapo hatalipwa fedha zake. Basi waumini waliwachwa vinywa wazi wasijue jinsi mhudumu yule walivyopatana na mhubiri wake na mbona akakataa na mkopo wake.

Basi kukopa harusi kulipa matanga. Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be