KAKAMEGA: Wakaazi Wazua Hofu Kuhusu Kudodora Kwa Usalama

Waendeshaji wa boda boda katika mji wa Kakamega. | picha: the-star.co.ke

Wakaazi wa Kakamega wamelalamikia kudorora kwa usalama na ongezeko la visa vya wahudumu wa bodaboda kunyang'anywa pikipiki zao na hata kuuawa.

Malalamishia haya yanafuatia mauaji ya wahudumu wawili wa bodaboda usiku uliopita licha ya serikali ya kaunti kutoa magari kwa idara ya usalama kupiga doria usiku.