Klabu 5 zinazolilia taji la klabu bingwa barani ulaya usiku na mchana

bayern.champions1
bayern.champions1
Taji la klabu bingwa barani ulaya ndilo taji kubwa ulimwenguni baada ya kombe la dunia ndani ya mchezo wa kandanda upande wa wanaume.

Dhamani ya taji hili limelifanya kuwa kwenye mstari wa kwanza kwa kila klabu inayoshiriki kwenye michuano hiyo kila msimu.

Kwa sasa kuna baadhi ya Vilabu barani ulaya ambavyo vimekuwa vikimwaga hela kama mchanga ili kuweza kunyakua taji hilo kwa miaka sasa.

  1. Manchester City

Miamba hawa wa soka nchini Uingereza wanamilikiwa na mwarabu ambaye kwa muda sasa amekuwa akifanya kila juhudi kuweza kuleta taji la UEFA ugani Etihad. Sheik alimlete Mhispaniola Pep Guardiola msimu wa kwanza ili kuongeza ushindani kwenye ligi kuu ya mabingwa barani ulaya. Ndani ya misimu mitatu sasa, Manchester City imetumia zaidi ya millioni mia tano kwa ajili ya kukisuka kikosi chao ili kuweza kushinda taji hilo. Usiku na mchana, Man- City inalilia taji la UEFA.

 2.  Paris Saint Germain

Wababe hawa wa Ufaransa  wametumia hela nyingi katika madirisha ya uhamisho kuliko klabu nyingine yoyote barani ulaya. PSG ilimsajili Neymar kutoka klabu ya Barcelona pamoja na Kylian Mbappe kutoka klabu ya monaco kwa zaidi ya pauni millioni mia nne. PSG imekuwa ikilisaka taji hili kwa zaidi ya mwongo mmoja sasa huku ikiwa imeshida mataji yote ya ligi kuu nchini Ufaransa na sasa hamu yao imebaki ni kulisaka taji la UEFA.

3. Juventus

Waitaliano hawa wamemleta mchezaji bora ulimwenguni Cristiano Ronaldo nchini Italia kwa ajili ya kuwasaidia kushinda taji la UEFA. Ronaldo aliwanyima miamba hawa wa italia taji hili kwa miaka miwili mfululizo kabla hajajiunga na waitaliano hawa mwaka 2017 pamoja na mwaka 2018. Kwa sasa ni zaidi ya miaka kumi na klabu ya Juventus haijawahi kuchukua taji hili.Juventus kwa sasa inaelekeza macho yote kwa taji hili kwa sasa na mikono yote.

4. Bayern Munich

Wajerumani hawa pia hawajakwepa mtego huu hata baada ya kushinda taji hili mwaka wa 2013. Bayern kwa sasa imerudi tena sokoni kwa ubaya ikilisaka taji hili baada ya kutumia kitita cha zaidi ya millioni mia tatu ili kukisuka kikosi chao kwa ajili ya michuano hii msimu ujao. Ujio wake phill Coutinho na Ivan Perisic ni baadhi ya majina makubwa makubwa ambayo Wajerumani hawa wameamua kuwaleta kwa ajili ya saka saka za klabu bingwa barani ulaya. Bayern Pia wana njaa ya kombe hili.

5.Atletico Madrid

Wengi watasema kuwa Barcelona ina njaa ya kuifikia Real Madrid katika kushinda mataji ya klabu bingwa barani ulaya ila tukiangazia kwa udani Klabu ya Atletico Madrid ndiyo iliyo na hamu ya kushinda taji hili kwa sana. Atletico imefika fainali ya taji hili mara mbili huku mara zote zikikuja mikononi mwa Real Madrid. Atletico ilimsajili kiungo mshambulizi wa Benfica ili kuweza kuwasaidia kushinda taji hili msimu ujao. Hamu yao imo juu ya klabu ya Barcelona.