unnamed (4)

Kocha wa Harambee Francis Kimanzi ajipata katika njia panda

Timu ya Taifa Harambee Stars ambayo inatarajiwa kuchuana na timu ya Uganda maarufu zaidi kama “the cranes” jumapili hii huenda ikakosa huduma ya Jesse Were baada ya kuripotiwa kupata jeraha wiki iliyopita.

Were ambaye anaichezea klabu ya Zesco united akiwa ameifungia klabu hiyo mabao 18, alipata jeraha hilo wakicheza dhidi ya Zanaco FC.

Jesse Were arudishwa kwenye kikosi cha Harambee stars

Kocha wa Harambee stars Francis Kimanzi amesema kuwa jeraha la Were ni pigo kwa timu hiyo lakini pia ni fursa kwa wachezaji wengine kuwakilisha timu ya taifa katika mechi hiyo. Kimanzi anaimani kuwa wachezaji ambao wamesalia watacheza vizuri huku akiwataka mashabiki wasiwe na hofu lolote.

Francis Kimanzi akabidhiwa mikoba ya Harambee stars kwa miaka miwili

Aidha mshambulizi Michael Olunga ambaye anaichezea klabu iliyo nchini Japan atashikilia nyadhfa ya unahodha huku akisaidiwa na Joash Onyango. Wachezaji wengine ambao huenda watakosa kucheza mechi hiyo ni Victor Wanyama, Joseph Okumu, Bernard Ochieng na John Avire.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments